FAQ   |   Webmail
  • All children have equal rights
  • All children should be encouraged to fulfill their potential
  • Everybody has a responsibility to support the care and protection of children.
  • The child's views should be taken into account where major decisions are to be made about his or her future
  • Organizations working with children have a duty to care for children
Recent News
Events Calendar

Print
SHUJAA JUKWA FORUM

AGYW Zaidi ya 100 walishiriki katika mkutano SHUJAA JUKWA FORUM  uliojumisha Viongozi wa serikali,Waakilishi kutoka taasisi binafsi na Viongozi wa Dini.Lengo kuu ni kujadili,Kujifunza ,,kuhamasika kupitia mafanikiowalioyapata AGYW kupitia mradi wa SAUTI unaotekelezwa na KIWOHEDE kupitia ufadhili wa JHPIEGO 
Katika tukio la SHUJAA JUKWAA FORUM lililofanyika tarehe 11/04/2019 Kyela.
Kupitia kupitia mradi huu wa SAUTI mafanikio mafanikio yameonekana amabayo yameleta hamasa kw Jamii,viongozi wa serikali na wadau wote wa maendeleo na kuwapongeza watoto kwa kwa elimu /mafunzo walioyapata KIWOHEDE kupitia SAUTI.  Baadhi ya matukio yaliyoibua  HISIA /hamasa kwa wadau walifika SHUJAA JAMII FORUM ni :
Binti wa form one kutokana na Ugumu wa maisha (Umaskini) alijiingiza katika biashara ya kuunza mwili ili  aweze kulisha familia /Wadogo zake ,Lakini sasa baada ya kupata mafunzo anabiashara yake , ameolewa na anatumia uzazi wa Mpago.
Binti mchamungu aliwahi kushiriki mapenzi kwa mara moja tu kumbe mwanaume aliyeshiriki naye alikuwa na maambukizi ya VVU ila kupitia huduma za upimaji pamoja na Ushauri nasaha binti huyu mdogo kabisa aligundulika ana VVU na sasa anatumia dawa na anafanya biashara zake mwenywe.
Binti aliyetoka katika mazingira magumu akiwa haina matumaini yeyote akisubiria kuolewa tu ili maisha yaende ila baada ya kupata mafunzo KIWOHEDE kupitia Mradi wa SAUTI  sasa ana mtaji wenye Zaidi ya laki 9 pia ana bodaboda  inayofanya kazi na kumuingizia kipato kila siku na anahamazisha mabinti wenzake .
Hawa ni baadhi tu ya Mabinti wanaonufaika na MRADI huu wa SAUTI kupitia KIWOHEDE.


Copyright © 2020 KIWOHEDE. All Rights Reserved.